Habari mpya

Miili ya waliotoweka miaka 16 iliyopita yapatikana

LoweImage copyrightAlex Lowe Foundation
Image captionAlex (kushoto) akiwa na Anker
Miili ya wakwea milima wawili kutoka Marekani waliotoweka katika milima ya Himalaya miaka 16 iliyopita imepatikana.
Mkwea milima maarufu duniani Alex Lowe alikuwa akikwea katika kilele cha Shishapangma chenye urefu wa 8,013m (26,290ft) eneo la Tibet Oktoba 1999 akiwa na mpiga picha David Bridges mkasa ulipotokea.
Wawili hao walifukiwa na maporomoko ya theluji.
Miili yao ilionekana na wakwea milima wawili wiki iliyopita ikiwa bado imekwama kwenye theluji.
LoweImage copyrightALEX LOWE FOUNDATION
Image captionLowe alikuwa mkwea milima stadi
Bw Lowe, 40, alitambuliwa kama mmoja wa wakwea milima stadi zaidi wa kizazi chake na aliokoa wakwea milima wengi sana milimani.
Yeye na Bridges, 29, walikuwa marafiki wakuu na walikuwa wakitafuta njia mpya ya kukwea mlima Shishapangma , mlima wa 14 kwa urefu duniani.
Mkewe Lowe, Jennifer Lowe-Anker, amesema kupatikana kwa mwili wa mumewe kutasaidia familia yake kutulia.
Jennifer baadaye aliolewa na Conrad Anker mwaka 2001.
Image copyrightALEX LOWE FOUNDATION
Anker alikuwa na wakwea milima hao wawili wakati wa mkasa lakini alinusurika akiwa na majeraha madogo.
Baadaye, yeye na wenzake wengine walitafuta wawili hao kwa siku nyingi bila mafanikio.
chanzo: BBC

No comments

+255716829257