MAAJABU: WALIOFARIKI KUPIGA KURA URUSI..
Msomi mbishani kutoka Urusi amependekeza mamilioni ya watu waliofariki wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia nchini humo wapewe kadi za kupigia kura.
Alexander Ageyev anasema hilo litawawezesha „kuendelea kuwa na usemi katika maendeleo ya taifa hilo”.
Ageyev ni mkurugenzi wa Taasisi ya Mikakati ya Kiuchumi ambayo ni sehemu ya Akademia ya Sayansi na kutokana na cheo chake, pendekezo lake limeangaziwa sana kwenye vyombo vya habari.
Moja ya mambo yanayojadiliwa sana ni: wafu watapiga kura vipi?
Ageyev amenukuliwa na gazeti la Fontanka akipendekeza kwamba marehemu wanaweza kupigiwa kura na watoto au wajukuu wao.
Pendekezo hilo limetolewa baada ya kufanyika mara ya pili kwa maandamano ya jamaa za waliofariki wakati wa vita hivyo, wajulikanao kama Immortal Regiment, wakiwa wamebeba picha za marehemu katika uwanja wa Red Square mjini Moscow.
Maandamano yamekuwa sehemu ya maadhimisho rasmi ya kila mwaka yanayoandaliwa tarehe 9 Mei.
Mwaka huu, Rais Vladimir Putin alihudhuria.
Katika uliokuwa Muungano wa Usovieti, watu zaidi ya 20 milioni walifariki wakati wa vita hivyo vilivyodumu kuanzia 1939 hadi 1945.
CHANZO: BBC
No comments
+255716829257