Habari mpya

Liverpool yaingia fainali ya ligi ya Uropa..

article-3575783-33E1BB8200000578-207_964x402
Klabu ya Liverpool imefanikiwa kuingia hatua ya fainali ya ligi ya Uropa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Villarreal.
article-3575783-33E1BB8200000578-207_964x402Wakiwa nyuma kwa bao moja katika mchezo wa awali,Liverpool walisawazisha matokeo baada ya Bruno Soriano kujifunga. Daniel Sturridge aliongeza bao la pili baadae na kuanza kuidididmiza timu hiyo kutoka Uhispania baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Roberto Firmino.
33E0432E00000578-0-image-a-21_1462476239477
33E0432E00000578-0-image-a-21_1462476239477
33E046AA00000578-0-image-a-19_1462476234496
Baada ya mchezaji wa Villareal Victor Ruiz kutolewa kwa kadi nyekundu,Adam Lallana alipigilia msumari wa mwisho na kuwa 3-0. Klopp ambaye amechukua timu hiyo kutoka kwa Brendan Rodgers mwezi Oktoba mwaka jana ameshaifikisha Liverpool katika fainali mbili huku ya kwanza ikiwa katika kombe la ligi ambapo walipoteza dhidi ya Manchester City.
Kwa matokeo hayo watakutana katika fainali na mabingwa watetezi Sevilla mjini Basel Mei 18 baada ya kuwacharaza Shakhtar Donetsk 5-3 na kuwa na ushindi wa jumla wa mabao5.
source: bongo5

No comments

+255716829257