Habari mpya

HIZI HAPA HABARI KUBWA ZAIDI ULIMWENGUNI LEO MEI 6..

Miongoni mwa habari nyingine kuu leo, Paul Ryan amesema bado hamuungi mkono Donald Trump, Canada nayo inawahamisha maelfu ya watu na Grim Sleeper amepatikana na hatia.

1. Shambulio Syria huenda ni ‘uhalifu wa kivita’

Watu 30Image copyrightSyria Civil Defence
Image captionWatu 30 walifariki kwenye shambulio hilo
Afisa wa cheo cha juu wa Umoja wa Mataifa anasema kuwa shambulizi la angani katika kambi moja ya wakimbizi nchini Syria, linalohofiwa kusababisha vifo vya watu 30, huenda likaorodheshwa kuwa uhalifu wa kivita.
Mkuu wa kitengo cha misaada cha Umoja wa Matiafa, Stephen O'Brien ametaka uchunguzi ufanyike kuhusu shambulizi hilo katika eneo lililo karibu na mpaka wa Uturuki.
Wenyeji wa eneo hilo, wameilaumu serikali ya Syria, ambayo ilikuwa ikiwalenga waasi katika eneo hilo.

2. Canada yajaribu kuwaokoa wakazi Alberta

MotoImage copyright
Image captionKuna wasiwasi huenda waliohamishwa wakafikiwa na moto
Serikali ya Canada imeanza operesheni kabambe ya kuwaokoa maelfu ya watu kwa kutumia ndege, ambao wameachwa bila makao kutokana na moto mkubwa wa porini katika mkoa wa Alberta.
Waokoaji wameonyesha hofu yao kuwa huenda walioathiriwa wakakwama tena, iwapo upepo mkubwa unaovuma utabadili mwelekeo wake.

3. Paul Ryan akataa kumuunga mkono Trump

RyanImage copyrightGetty
Image captionRyan amesema sharti Trump aoneshe kwamba anasimamia maadili ya chama hicho
Spika wa bunge la wawakilishi nchini Marekani ambaye pia ni mwanachama wa Republican Paul Ryan anasema kuwa hayuko tayari kumuunga mkono Donald Trump kama mwaniaji wa urais kwa tiketi ya chama hicho.
Bw Ryan anasema kuwa itambidi mwanabiashara huyo bilionea kuonyesha wazi kuwa anaunga mkono kanuni za chama hicho.

4. Spika wa Bunge atimuliwa Brazil

CunhaImage copyrightReuters
Image captionCunha anadaiwa kuhujumu uchunguzi wa tuhuma dhidi yake
Mahakama ya Juu nchini Brazil imemsimamisha kazi spika wa Bunge la Congress, ambaye aliongoza harakati za kumvua mamlaka rais Dilma Rousseff.
Spika huyo Eduardo Cunha anashtumiwa kuwa kizuizi cha uchunguzi dhidi ya tuhuma za ufisadi zinazomkabili.

5. Tajiri wa Panama akamatwa Colombia

WakedImage copyrightAFP
Image captionWaked amekuwa akitafutwa na maafisa Marekani
Colombia imemekamata kiongozi wa himaya moja ya kibiashara Panama kwa shutuma za utakatishaji wa fedha chafu.
Mamlaka nchini marekani inasema kuwa Nidal Waked alitumia biashara zake za benki na uuzaji wa mali isiyohamishika kusaidia walanguzi wa dawa za kulevya kusafisha fedha chafu.

6. Mkutano wa chama tawala waanza Korea Kaskazini

KimImage copyrightAP
Image captionNi mkutano wa kwanza mkuu kuongozwa na Kim Jong-un
Nchini Korea Kaskazini kongamano la kwanza kubwa zaidi la chama tawala cha Workers Party linatarajiwa kuanza baadaye mjini Pyongyang.
Hotuba ya kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-un inatarajiwa kutawala ufunguzi wa kongamano hilo.
Mwandishi wa BBC mjini Pyongyang anasema huenda Bw Kim akatumia fursa hiyo kutetea na kusisitiza matamanio yake ya zana za kinyuklia.

7. Grim Sleeper apatikana na hatia

Mahakama nchini marekani imempata na hatia muuaji wa watu wengi anayejulikana kama Grim Sleeper, aliyetekeleza mauaji ya wanawake 9 pamoja na msichana mwenye umri wa miaka 9 mjini Los Angales.
Jopo la waamuzi lilipokea ushahidi wa jinsi mwanamme huyo Lonnie David Franklin Junior, alivyotupa miili ya waathiriwa wake 'kwenye mapipa ya takataka na vichochoroni.
Anatarajiwa kuhukumiwa baadaye.

No comments

+255716829257