Habari mpya

Dr Asha RoseMigiro ateuliwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

MigiroImage copyrightAsha Migiro Twitter
Image captionBi Migiro alihudumu kama Waziri wa Katiba na Sheria serikali iliyopita
Aliyekuwa miongoni mwa waliokuwa wakipigania tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha Mapinduzi katika uchaguzi uliopita ameteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Dkt Asha-Rose Migiro atachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw Peter Kallaghe ambaye amerejea nyumbani.
Anatarajiwa kuapishwa Alhamisi katika ikulu ndogo ya rais Dodoma.
Bi Migiro alihudumu kama Waziri wa Katiba na Sheria serikali iliyopita na alikuwa miongoni mwa wagombea watatu waliokuwa wamesalia kwenye kinyang'anyiro cha kuteua mgombea wa CCM uchaguzi wa mwaka jana, kabla ya mwishowe Dkt John Magufuli kuidhinishwa.
Mgombea huyo mwingine alikuwa Balozi Amina Salum Ali.

No comments

+255716829257