Diamond na Theo Mafikizolo kuchuana kwenye kipindi cha Lip Sync Battle Africa May 26
Diamond Platnumz na msanii wa kundi la Mafikizolo, Theo, watachuana kwenye kipindi cha Lip Sync Battle Africa kinachorushwa na kituo cha runinga cha MTV Base na MTV SA.
Kwenye kipindi hicho, wasanii wawili hushindana kuziimba nyimbo za wasanii wengine kwa kugandamizia na kupatikana mshindi mmoja. Show ya Diamond na Theo itaruka May 26.
“Lip Sync Battle Africa this coming Thursday26 May 2016 #teamtheo Vs #teamdiamond it’s a SHOWDOWN Africa vote #teamtheo microphone as a take on my Tanzanian brother @diamondplatnumz Pls don’t forget to tag @mtvza @mtvbaseafrica @lsbafrica,” ameandika Theo kwenye Instagram.
Lip Sync Battle ni show iliyoanzia Marekani na kuongozwa na rapper LL Cool J na mke wa John Legend, Chrissy Teigen.
Kwa Afrika show hiyo inaongozwa na mrembo wa Afrika Kusini Pearl Thusi na staa wa Nigeria, D’Banj.
No comments
+255716829257