Habari mpya

Atletico Madrid yatinga fainali ligi ya mabingwa

GriezmannImage copyrightReuters
Image captionGriezmann alifungia Atletico bao la kusawazisha
Klabu ya soka ya Atletico Madrid imefanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha miaka mitatu baada ya kupata bao la ugenini walipokipiga dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani.
Atletico wakiwa na faida ya bao la nyumbani katika nusu fainali ya kwanza nchini Uhispania, Bayern walisawazisha kupitia mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa na Xabi Alonso kwenye mechi ya Jumanne iliyochezewa uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Arena.
Mlinda mlango wa Atletico Jan Oblak aliokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Thomas Muller kabla ya mshambuliaji Antoine Griezmann kusawazisha na kuwa 1-1.
MadridImage copyrightEPA
Image captionAtletico Madrid wamefuzu kwa fainali itakayochezwa 28 Mei
Robert Lewandowski alifunga bao la pili baada ya kupokea pasi ya mpira wa kichwa kutoka kwa Arturo Vidal huku Atletico wakishindwa kusawazisha baada ya mkwaju wa penalti uliopigwa na Fernando Torres kuokolewa na mlinda mlango Manuel Neuer.
Matokeo ya jumla ya nusufainali hiyo yalimalizika sare 2-2 lakini Madrid wakasonga kwa kuwa na bao la ugenini.
Sasa Atletico watakutana na mshindi wa mchezo kati ya Real Madrid na Manchester City utakaopigwa kesho dimbani Santiago Bernabeu katika fainali mjini Milan tarehe 28 Mei.

No comments

+255716829257