Habari mpya

Wanajeshi wa Amisom waua watu wanne Somalia

AmisomImage copyrightAFP
Image captionWanajeshi wa Amisom wamekuwa wakikabiliana na wapiganaji wa al-Shabab
Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (Amisom) wamewaua watu wanne viungani mwa mji wa Bulla Marer kusini mwa Somalia, wakazi wa eneo hilo wanasema.
Waliouawa ni pamoja na mwanamke mkongwe na mtoto wa umri wa miaka tisa.
Wakazi wa mji huo ulioko jimbo la Lower Shabelle wameandamana mjini kushutumu mauaji hayo.
Kwa mujibu wa wakazi, wanajeshi waliouawa walikuwa kwenye gari ndogo waliposimamishwa na wanajeshi wa Amisom, kuamriwa watoke nje na kisha wakapigwa risasi.
Abdiwahid Maalim Ibrahim, ambaye ni mwanawe ajuza aliyeuawa na babake msichana aliyeuawa, ameambia idhaa ya Kisomali ya BBC kwamba watu hao waliouawa walikuwa wakielekea Mogadishu kutafuta matibabu.
“Mapema leo, mamangu aliyekuwa na umri wa miaka 80 na binti yangu wa miaka tisa walikuwa wakiugua na waliondoka Bulla Marer wakitumia gari lililokuwa likiendeshwa na marafiki zangu wawili kuelekea Mogadishu,” amesema Ibrahim.
"Wanajeshi wa Amisom waliwasimamisha viungani mwa mji na kuwaua wote.”
AmisomImage copyrightAFP
Image captionWanajeshi wa Amisom husaidia serikali ya Somalia
Kikosi cha Amisom kimethibitisha kwamba kuna watu wanne waliouawa lakini kikasema hawakuuawa makusudi.
Msemaji wa Amisom Kanali Joe Kibet, ameambia BBC Somali kwamba dereva wa gari hilo alikaidi agizo la kusimama.
Tarehe 31 Julai, 2015 wanajeshi wa Amisom waliauwa raia kadha harusini katika mji wa Marka, kusini mwa Somalia kisa kilichoshutumiwa vikali.

No comments

+255716829257