Habari mpya

Shabiki kujishindia pauni 20,000 Leicester ikishinda ligi

Image captionLeigh Herbert shabiki wa Leicester
Shabiki mmoja wa timu ya Leicester amesema kuwa ana uhakika klabu hiyo itashinda ubingwa wa ligi na kumfanya kupata zaidi ya pauni 20,000.
Leigh Herbert aliwekeza 5000 baada ya kupata vinywaji kadhaa wakati wa likizo huko Newquay ,Cornwall mwaka uliopita.
Image copyrightReuters
Image captionClaudio Ranieri
Nina furaha tele kwa sababu nina uhakika wa asilimia 100 kwamba hilo litafanyika.
Leigh alicheza kamari hiyo kufuatia uteuzi wa mkufunzi Claudio Ranieri.''Nilifikiria kwamba atailetea kilabu hiyo kitu maalum''.
''Nilijua kwamba kutokana na uzoefu alionao kuna kitu kitafanyika''.Na kulingana na mambo yalivyo kwa sasa Leigh alikuwa na haki kuwa na matumaini.
Image copyrightGetty
Image captionWachezaji wa Leicester
Iwapo timu yake itaishinda Manchester United ama Spurs ishindwe na wapinzani wake wa jadi Chelsea wikendi hii,Leicester watakuwa mabingwa na Leigh atajipatia pauni 20,000.
chanzo: BBCmichezo.

No comments

+255716829257