Habari mpya

Ranieri: Leicester sio Man City au United

RanieriImage copyrightReuters
Image captionRanieri amesema hawataki kupoteza mwelekeo
Claudio Ranieri amesema iwapo klabu mbili za Manchester ndizo zingekuwa katika nafasi ambayo Leicester City kwa sasa wamo, basi wangu wangeamini mbio za ligi “zimeisha”.
Leicester, ambao watakuwa wenyeji wa West Ham Jumapili, wamo alama saba mbele kileleni mwa Ligi ya Premia zikiwa zimesalia mechi tano msimu huu.
Ranieri amesema Leicester, ikizingatiwa kwamba walinusurika kushushwa daraja miezi 12 iliyopita, wamefanya makubwa sana msimu huu.
Hata hivyo amesema ni lazima washinde taji la ligi ndipo waweze kukumbukwa kwa “miaka 30 au 40 ijayo”.
"Hatujashinda chochote bado,” amesema Mwitaliano huyo mwenye umri wa miaka 64.
“Soka huwa na maajabu yake. Kama haungekuwa hapa Leicester lakini uko kwingine tuseme City au United, ukiwa na alama saba au zaidi mbele, ungesema ‘mambo yameisha’.
"Kwa sasa hauwezi kufikiria hivi. Kisa? Sisi ni eicester. Lazima tupambane na tuwe na mwelekeo na kuwa thabiti.
Leicester wameshinda mechi zao tano zilizopita bila kufungwa bao.
Iwapo watashinda mechi tatu zijazo basi watatwaa taji la ligi.
SunderlandImage copyrightGetty
Image captionLeicester walilaza Sunderland 2-0
Ushindi wao wa 2-0 ugenini Sunderland Jumapili uliwahakikishia kumaliza katika nafasi nne za kwanza.
Mambo makubwa yasipofanyika, kwa mfano Manchester City na Liverpool kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na Europa League, basi wamehakikishiwa kucheza hatua ya muondoano wa kufuzu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
source: BBC

No comments

+255716829257