Habari mpya

Machar awekewa masharti ya kuingia Juba

Image copyrightAFP
Image captionRais Salva Kiir
Sudan Kusini inasema kuwa kiongozi wa waasi Riek Machar hawezi kwenda mji mkuu Juba hii leo.
Waziri wa habari alisema kuwa serikali itatoa tu kibali kwa ndege itakayombeba Machar baada ya waangalizi kubaini kiasi cha silaha wafanyikazi wake watakuwa nacho.
Machar kwa sasa yuko nchini Ethiopia
Image copyrightReuters
Image captionRiek Machar
Siku ya Ijumaa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon alitoa wito kwa Machar kurejea nchini Sudan Kusini bila kuchelewa.
source: BBC

No comments

+255716829257