Habari mpya

Kesi dhidi ya unyanyasaji wa CIA kuendelea US

Image copyrightGetty
Image captionMkurugenzi mkuu wa shirika la kijasusi la Marekani CIA John Brennan
Jaji nchini Marekani ameruhusu kuendela kwa kesi inayohusu mateso yanafayonywa na shirika la ujasusi la Marekani CIA dhidi ya kile kinachotajwa kuwa vita dhidi ya ugaidi
Chama cha kutetea maslahi ya umma kiliwashtaki wanasaikolojia wawili kwa niaba ya waliokuwa wafungwa watatu wa CIA na kuwalaumu kwa kutoa mafunzo kuhusu mbinu za kutesa
Wakijitetea wanasaikolojia hao walisema kuwa walibuni programu hiyo lakini hawakuhusika kuitekeleza.
Zaidi ya wafungwa 100 walifanyiwa mbinu hizo za mateso ikiwemo kunyimwa usingizi, kumwagiwa maji na kupigwa.
chanzo: BBC

No comments

+255716829257