Habari mpya

Gari linalojiendesha la Google lagonga basi

Image copyrightAP
Image captionGari la Google linalojiendesha
Gari moja la Google linalojiendesha liligonga basi moja mjini California mwezi uliopita.Hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Sio mara ya kwanza kwa gari linalojiendesha la kampuni ya Google kuhusika katika ajali,lakini huenda ni mara ya kwanza kwa magari hayo kufanya ajali.
Kampuni ya Google inataraijiwa kukutana na idara ya magari mjini California ili kuzungumzia kuhusu kisa hicho na kubaini ni nani wa kulaumiwa.
Mnamo tarehe 14 mwezi Februari gari hilo ambalo lilikuwa likisafiri kwa kasi ya kilomita 3 kwa saa liligonga basi moja la umma lililokuwa likisafiri kwa kasi ya kilomita 24 kwa saa.
Mtu aliyekuwa katika gari hilo la Google aliripoti kwamba alidhani basi hilo lingepunguza mwendo ili kuisubiri gari hiyo kupita hivyobasi hakuingilia kompyuta inayoendesha gari hilo.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Mountain View karibu na makao makuu ya kampuni ya google.
Katika taarifa yake Google ilisema:Tunabeba lawama kwasababu iwapo gari letu lisingeenda kusingekuwa na ajali.

No comments

+255716829257