Habari mpya

Zimbabwe yanasa ndege na mamilioni ya rand

Image copyrightkwa Hisani
Image captionNdege hiyo aina ya MD-11 trijet ilikuwa inaelekea Afrika Kusini ikiwa na mamilioni ya Rand (Sarafu ya Afrika Kusini).
Zimbabwe imekamata ndege moja ya Marekani iliyopatikana imebeba mamilioni ya pesa na maiti ya mtu mmoja.
Wafanyikazi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare, wanasema waligundua damu ilikuwa ikivunjwa kutoka kwa ndege moja ya kibinafsi iliyotua ikiomba kuongeza mafuta.
Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika dogo la ndege la Western Global Airlines ilisajiliwa nchini Marekani.
Yamkini ndege hiyo ya kibinafsi ilikuwa ikitoka Ujerumani ikielekea Afrika Kusini.
Mkuu wa halmashauri inayosimamia viwanja vya ndege vya Zimbabwe David Chawota anasema mamilioni ya pesa iliyopatikana katika ndege hiyo ni mali ya benki kuu ya Afrika Kusini.
Shirika la habari la FIn24la Afrika kusini linasema kuwa ndege hiyo sasa imekamatwa ilikuruhusu uchunguzi wa kina ufanyike.
''kama mnavyofahamu swala hili linahusu watu wa mataifa mengine na ndege inayomilikiwa na kampuni iliyosajiliwa huko Marekani kwa hivyo tayari hii ni swala linalohusu serikali kuu'' alisema Chawota.
Msemaji wa polisi Charity Charamba alithibitisha tukio hilo.
Gazeti la serikali Herald lilimnukuu afisa mmoja aliyethibitisha kuwa ndege hiyo aina ya MD-11 trijet ilikuwa njiani kuelekea Afrika Kusini ikiwa na mamilioni ya Rand (Sarafu ya Afrika Kusini).
Image captionZimbabwe yanasa ndege na mamilioni ya rand
Kulingana naye rand milioni moja ni sawa na dola elfu sitini na mbili za Marekani $62,500.
Abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo walikuwa ni Wamarekani wawili raia mmoja wa Afrika Kusini na Mpakistani .
Magari kadhaa ya ubalozi wa Marekani yalionekana mapema leo yakiingia na kutoka katika uwanja huo.

No comments

+255716829257