Waliowabaka wanawake Cologne huenda wasikamatwe
Wengi wa wanaume waliowabaka wanawake katika mji wa Cologne wakati wa sherehe za mwaka mpya huenda wasikamatwe, ameeleza mkuu wa polisi mjini humo.
Akizungumza na BBC, afisa huyo, Juergen Mathies amesema kuwa picha za video zilizonaswa na mtambo wa CCTV hazikua nzuri vya kutosha kuwezesha kutambuliwa kwa uhalifu wa kingono.
Maafisa wa usalama wameweza kuwatambua washukiwa 75. Wengi ni kutoka Afrika magharibi walioingia Ujerumani kinyume cha sheria ama kutafuta hifadhi.
Zaidi ya malalamiko 500 ya uhalifu yaliwasilishwa kwa polisi, ambapo asilimia 40% yalidaiwa kuwa ni ya ubakaji.
"picha za CCTV si bora kiasi cha kuonyesha wazi vitendo vya ubakaji. Tunaweza kuona baadhi ya vitendo vya wizi, lakini ni hilo tu.
''Tunategemea maelezo ya mashahidi na waathiriwa wanaowatambua walio washambulia," alisema Bwana Mathies.
Raia wawili wa Morocco na mtunisia wanatarajiwa kwenda mahakamani baadae kwa tuhuma za wizi, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mtu yeyote kuwahi kupelekwa mahakamani kuhusiana na wizi uliofanyika katika mashambulizi ya mwaka mpya mjini humo.
Wanaume kumi na watatu wamekwisha kamatwa kwa wizi, lakini ni mmoja tu mwenye umri wa miaka 26 raia wa Algerian anaeomba hifadhi ya ukimbizi aliekamatwa kwa akishukiwa kwa ubakaji.
No comments
+255716829257