Habari mpya

Thomas Emmanuel Ulimwengu aotea

Katika Afrika ya Kati kulikuwa na Mechi ya Ligi ya Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo nyasi za Uwanja wa Frederic Kibassa Maliba mjini Lubumbashi zilikuwa zinawakutanisha wafalme wa Ligi ya Mabingwa Afrika TP Mazembe dhidi ya FC Saint Eloi Lupopo lakini hakuna aliyeliona lango la mweziye ijapokuwa Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu alitikisa nyavu kwa Kichwa lakini kumbe alikuwa tayari ameotea. TP Mazembe sasa wanachangamsha misuli kujiandaa na mechi ya Super Cup ya Afrika dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia mabingwa wa Kombe la Shirikisho.

No comments

+255716829257