Habari mpya

Seli za ndege zenye tiba ya maambukizi

Image captionFungus ya ndege
Seli zenye kinga maalum zinazopatikana katika ndege zina uwezo wa kuangamiza maambukizi yanayodaiwa kusababisha vifo miongoni mwa maelfu wa binaadamu kila mwaka ,wanasayansi wamedai.
Maambukizi ya Cryptococcus neofarms husababisha vifo miongoni mwa watu wenye kinga dhaifu hususan wale walio na ugonjwa wa HIV.
Ndege hubeba maambukizi hayo ,huku wataalam wakishangaa ni kwa nini ndege wenyewe hawapatikani na ugonjwa huo.
Utafiti umebaini kwamba seli ya damu inayojulikana kama Macrophage inaweza kuzuia ukuaji wake.
Maambukizi hayo yanayopatikana katika mavi ya ndege hususan huambukiza mapafu na mfumo mkuu wa neva.
Wanasayansi katika chuo kikuu cha Sheffield pamoja na kile cha Birminghan walibaini kwamba maambukizi hayo hukuwa polepole katika njia ya utumbo,lakini kila yanapojaribu kuvamia kinga ya mwili ya ndege kinga hiyo uyaharibu.
Daktari Simon Johnston ambaye aliongoza utafiti huo,alisema:Ndege wana joto la juu mwilini ikilinganishwa na binaadmu lakini hilo halitoshi kuangamiza maambukizi hayo.
Kwa kuchunguza seli za ndege katika mashine ya microscopy,tumebaini kwamba seli hizo zina uwezo wa kuangamiza ukuaji wa maambukizi hayo ambayo huwauwa binaadamu.

No comments

+255716829257