Paul Scholes mapenzi yake kwa Man United yanataka kumuachisha kazi BT Sport ili …
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Man United na timu ya taifa ya Uingereza Paul Scholes ambaye amewahi kuichezea klabu ya Man United kwa zaidi ya miaka 15, anatajwa kutaka kuacha kazi yake ya uchambuzi wa soka katika kituo cha BT Sport kwa ajili ya mapenzi yake kwa Man United.
Scholes anataka kuachana na kazi ya uchambuzi ili ajiunge kwa mara nyingine tena na klabu ya Man United, ila safari hii anataka kurudi kama kocha wa timu hiyo na sio mchezaji, Scholes ni moja kati ya wachambuzi wanaokosoa sana mbinu za kocha waMan United wa sasa Louis van Gaal.
Scholes aliwahi kuwa moja kati ya watu wa benchi la ufundi la Man United na kumsaidia rafiki yake Ryan Giggs kuifundisha Man United katika kipindi kifupi cha mpito, April 2014 baada ya Man United kumfuta kazi kocha wa zamani wa Man United David Moyes, ilaManchester Evening news wanaripoti kuwa sasa anataka kurudi serious katika kazi hiyo.
source:millardayo.com..http://millardayo.com/scholes56-2/
No comments
+255716829257