Habari mpya

MOJA KWA MOJA: Yanayojiri Uganda

14:09 Kizza Besigye na rais wa FDC Mugisha Muntu wamekamatwa katika makao makuu ya chama hicho Najjanankumbi, kituo cha televisheni cha NBS kimeripoti. Polisi wametumia mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa chama hicho.
13:00 Ripoti zinasema makao makuu ya chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) yamevamwia na maafisa wa usalama.
12:35 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Badru Kiggundu anatarajiwa kutangaza matokeo mengine mwendo wa saa nane unusu adhuhuri.
11:50 Mitandao ya kijamii nchini Uganda bado imefungwa kwa siku ya pili. Kwa muda mfupi usiku, watu waliweza kuingia mitandao hiyo lakini asubuhi hawakuweza. Jana Rais Museveni alisema hatua hiyo ilichukuliwa kwa sababu za kiusalama.
11:26 Tume ya Uchaguzi imetoa mkumbo wa pili wa matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais ambayo yanaonesha Rais Yoweri Museveni ameweka pengo la kura milioni moja kati yake na Dkt Kizza Besigye.
Matokeo kwa sasa ni kama ifuatavyo:
Matokeo kwa sasa (Vituo 10,246 kati ya 28,010)
Abed Bwanika35,487
Amama Mbabazi60,694
Baryamureeba Venasius23,380
Benon Biraaro11,176
Kizza Besigye1,182,025
Joseph Mabirizi10,266
Maureen Kyalya18,444
Yoweri Museveni2,191,283
Chanzo: Tume ya Uchaguzi Uganda (EC)
08:25 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Badru Kiggundu anatarajiwa kutangaza mkumbo wa pili wa matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais.
Matokeo ya mkumbo wa kwanza kutoka kwa tume hiyo ya uchaguzi yanaonesha Rais Museveni anaongoza akifuatwa na Dkt Kizza Besigye. Matokeo ni kutoka vituo 6,448 kati ya 28,010
  • Abed Bwanika 22,180 (1.0%)
  • Amama Mbabazi 41,291 (1.87%)
  • Baryamureeba Venasius 15,260 (0.69%)
  • Benon Buta Biraaro 7,228 (0.33%)
  • Kizza Besigye 738,628 (33.47)
  • Mabirizi Joseph 6,833 (0.31%)
  • Maureen Kyalya 12,742 (0.58%)
  • Yoweri Museveni 1,362,961 (61.75%)
07:05 Mgombea urais wa chama cha FDC Dkt Kizza Besigye yuko huru baada yakukamatwa na kuzuiliwa kwa muda na maafisa wa polisi jana.
Besigye pamoja na meya wa zamani wa Kampala Elias Lukwago walifika katika kile polisi wanasema ni jumba lao eneo la Naguru, Kampala na kutaka kuingia ndani kufanya ukaguzi. Dkt Besigye na wenzake walidai kilitumiwa kuiba kura. Polisi wamekanusha hayo.
Msemaji wa polisi wa Kampala Patrick Onyango amesema ni mkuu wa polisi pekee anayeweza kutoa idhini kwa mtu kuingia ndani.
“Dkt Kizza Besigye alikamatwa kwa kujaribu kuingia eneo lisiloruhusiwa na baadaye aliachiliwa kwa bondi ya polisi. Alipelekwa nyumbani kwake Kasangati. Uchunguzi zaidi kuhusu kisa hiki unaendelea,” alisema kupitia taarifa.
Image captionBesigye akiwa hoteli ya Imperial Royale, Kampala baada ya kuachiliwa huru
07:50 Hujambo! Twatumai umeamka salama na buheri wa afya. Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu yanayojiri nchini Uganda baada ya uchaguzi mkuu kufanyika hapo jana.

Kura zinaendelea kuhesabiwa katika maeneo mengi. Katika baadhi ya vituo mjini Kampala na wilaya ya Wakiso ambapo uchaguzi ulitatizika, upigaji kura utaendelea leo.

No comments

+255716829257