Mafuta yapanda bei asilimia 6,000% Venezuela
Venezuela imeongeza bei ya Petroli kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20.
Rais Nicolas Maduro ametangaza bei mpya ya mafuta ambayo itakuwa senti sitini kwa dola ($0.60).
Maduro anasema kuwa bei hiyo ya mafuta ndio itakuwa ya chini zaidi duniani.
Bei ya mafuta ya petroli ambayo sio ya kiwango cha juu itapanda kwa peni moja kwa dola ($0.10)
Rais huyo vilevile, ametangaza mabadiliko zaidi ya sera mpya za kiuchumi nchini Venezuela ikiwemo kuporomosha thamani ya sarafu ya nchi hiyo.
Wadaduisi wanasema kuwa kuongezwa kwa bei hiyo ya mafuta itaisaidia uchumi wa taifa hilo kuokoa takriban dola milioni 800 kila mwaka.
"Venezuela ndio itakayokuwa na mafuta yenye thamani ya chini zaidi duniani '' alisema bwana Maduro katika hotuba ya taifa kupitia kwa runinga ya taifa.
''Kwa kweli bei ya mafuta hapa nchini ni ya chini zaidi''
Hata hivyo mataifa mengine yanayozalisha mafuta kama Saudi Arabia yanamafuta ya bei ya chini mno.
Maduro alisema kuwa imewalazimu kupandisha bei ya mafuta ilikufidia maswala fulani ya bajeti ya taifa.
Mara ya mwisho serikali ilipotangaza nyongeza ya bei ya vyakula mwaka wa 1989 maandamano makubwa yalitibuka nchini humo maandamano yaliyopelekea mapinduzi yaliyoongozwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo marehemu Hugo Chavez.
Venezuela ni moja ya mataifa yaliyoathirika sana na kuporomoka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.
Mafuta inachangia asilimia 95% ya pato la taifa.
Pato la taifa lilizorota kwa zaidi ya asilimia kumi 10% mwaka uliopita.
No comments
+255716829257