Habari mpya

Kizza Besigye azuiliwa na polisi Uganda

BesigyeImage copyrightBBC World Service
Image captionDkt Kizza Besigye amegombea urais dhidi ya Museveni mara tatu awali
Mgombea urais wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa na maafisa wa polisi, watu walioshuhudia wanasema. Polisi hata hivyo wanasema "anazuiliwa tu" na ataachiliwa huru baadaye.
Uchaguzi mkuu utafanyika Alhamisi.
Gari lake lilikuwa likipitia barabara ya Jinja, mjini Kampala, msafara wake ukisindikizwa na mamia ya wafuasi, pale polisi walipotumia vitoa machozi kuwatawanya wafuasi hao na wakamkamata mwanasiasa huyo.
Bw Besigye alipangiwa kufanya mikutano ya kampeni leo mjini Kampala.
Ripoti zinasema anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Nagalama.
Mkuu wa Polisi Jenerali Uganda Kalekezi Kayihura amethibitisha kwamba polisi wamekabiliana na wafuasi wa upinzani lakini akakanusha habari kwamba Bw Besigye amekamatwa.
Hata hivyo amesema wafuasi kadha wa upinzani wanazuiliwa.
BBC
Image captionJenerali Kayihura
Maafisa wa polisi wameambia BBC baadaye kwamba ni kweli Bw Besgiye "anazuiliwa lakini hakukamatwa" na kwamba ataachiliwa huru baadaye na kuruhusiwa kuendelea na kampeni.
Wamesema alizuiliwa kwa sababu ya kutotii agizo la kutotatiza uchukuzi mjini.
Polisi



Image captionWafuasi kadha wa Besigye wamekamatwa na polisi
































No comments

+255716829257