Habari mpya

UTAFITI: KUNGUNI HAWASIKII DAWA.

Image captionUtafiti: Kunguni hawasikii dawa
Licha ya kuhusishwa na uchafu, na mazingira duni, kunguni ameibuka kuwa mdudu mwenye uwezo mkubwa wa kustahimili hatari dhidi ya maisha yake.
Utafiti mpya umebaini kuwa wadudu hao wanaweza kustahimili sio tu tanuri ya moto na baridi kali bali pia madawa ya kisasa ya kuua wadudu wanaotambaa.
Kunguni wamegundulika kuwa wanaweza kustahimili kupuliziwa dawa nyingi ya sumu kwa kuimarisha uwezo wake wa kujikinga dhidi ya sumu moja baada ya nyengine.
Wadudu hao ambao huishi kwa kufyonza damu ya wenyeji wake wakiwa usingizini wanauwezo mkubwa wa kibayolojia ya kujikinga dhidi ya sumu kali.
Hii ni kusema kuwa kadri vizazi vya kunguni vinavyopuliziwa madawa yenye sumu ndivyo wadudu hao wanavyoimarisha uwezo wake wakuzuia maafa miongoni mwa watoto wao.
Aidha, watafiti wanaema kuwa vipimo 1000 vya sumu kali aina ya (neo-nicotinoid) vinahitajika kuua kunguni mmoja huko Marekani katika majimbo ya Cincinnati na Michigan ikilinganishwa na maeneo mengine duniani.
Image captionWatafiti wanasema vipimo 1000 vya sumu kali vinahitajika kuua kunguni mmoja katika majimbo ya Cincinnati na Michigan ikilinganishwa na maeneo mengine duniani
Watafiti hao sasa wanasema kuwa kuna hatari kubwa ya mdudu huyo kuenea kote duniani kutokana na utandawazi na soko huria ambao umefanya ulimwengu kuwa kitongoji kikubwa tu.
Aidha wanasayansi hao wanashauri kutafutwa mbinu tofauti na mpya ya kukabiliana na kunguni pasi na kutumia sumu, kama vile kutafuta wadudu wengine wanaoweza kuwala ilikuzuia wadudu hao kuenea kote duniani.
Taarifa hiyo imechapishwa katika jarida la utabibu la The Journal of Medical of Entomology.

No comments

+255716829257