JE YAYA TOURE ALIKUWA SAHIHI??
Pierre Emerick Aubameyang amesema kuwa alihisi uchungu baada ya Yaya Toure kusema kwamba 'sio heshima' kwa yeye kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora barani Afrika mwaka uliopita.
Mchezaji huyo wa Manchester City alisema kwamba hatua hiyo ilileta aibu kwa bara la Afrika,huku mchezaji wa Swansea Andrew Ayew pia akihoji hatua hiyo.
Toure wa taifa la Ivory Coast na Ayew wa Ghana walifika katika fainali za kombe la Afrika huku Gabon ikitolewa mapema.
''Nilisikia uchungu sana na kile kilichosemwa'',alisema mshambuliaji huyo wa Borussia Dortmund Aubameyang.''Ni aibu''.
Katika kura iliopigwa na makocha na wakurugenzi wa kiufundi katika mataifa ya shirikisho la CAF,Aubameyang alipata kura 143,Toure akipata 136 huku Ayew akijipatia 112.
Toure,ambaye alitangazwa kuwa mchezaji bora wa 2015,alishinda tuzo hiyo kwa kipindi cha miaka minne iliopita mfululizo.
''Tuzo hiyo ni ya mwaka mzima na sio kutokana michuano ya kombe la bara Afrika pekee'',aliongezea Aubameyang, ambaye anaongoza kwa mabao katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani akiwa amefunga magoli 18.
No comments
+255716829257