Mkewe rais wa Marekani bi Michelle Obama amejiunga na mtandao wa kijamii wa Snapchat.
Bi
Obama alitangaza kujiunga na Snapchat siku chache kabla ya kufunga
safari ya Afrika ambako anatarajiwa kujiunga na wanaharakati wa naopigia
debe elimu ya mtoto wa kike .
Ziara hiyo ya itampeleka Liberia, Morocco na kisha Uhispani.
Mtandao huo unamruhusu kujumuika na walengwa wa mradi huo wa vijana.
Snapchat ni mtandao unaoruhusu habari picha na video kutoweka au kufutika baada ya saa 24.
Bi Obama alichapisha picha yake mwenyewe na kutangaza kuwa sasa amejiunga na kuwa yeye ni mmoja wao!
Mmoja wa maafisa katika afisi yake Kelsey Donohue, alizungumzia kujiunga kwake na Snapchat .Wachanganuzi
wanatarajia Bi Obama kupata wafuasi maradufu haswa mashabiki wake ambao
wanatarajia kuona picha za ndani ya ikulu ya White House na pia kitaru
chake kidogo mbali na habari kuhusiana na kampeini yake mpya ya
Let's Move!
Bi Obama atajiunga na wasanii Meryl Streep na Freida Pinto katika ziara hiyo barani Afrika.
Wanawe Malia na Sasha wataambatana na mama yao katika ziara hiyo.
Mkewe Obama anawafuasi 4.58m kwenye mtandao wa Twitter na 5m kwenye mtandao wa Instagram.
chanzo: BBC
MICHELLE OBAMA SASA YUPO SNAPCHAT..
Reviewed by Chimbuko Online
on
June 22, 2016
Rating: 5
No comments
+255716829257