Mabaki yanayokisiwa kuwa ya ndege ya Malaysia yapatikana TZ..

Maafisa wa uchukuzi wanachunguza iwapo mabaki ya ndege yaliyopatikana ufuoni ni ya ndege ya
Malaysia iliyotoweka miaka miwili iliyopita.
Picha za mabaki hayo yaliyopatikana visiwa vya Pemba zimekuwa zikisambaa sana mtandaoni.Hilo litawezekana tu wakati watengenezaji wa ndege hiyo watafika na kuchunguza mabaki hayo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uchukuzi wa Ndege Tanzania Redemptus Bugomola ameambia BBC kwamba bado ni mapema mno kubaini iwapo mabaki hayo ni ya ndege ya MH370.
Shirika la habari nchini Malaysia Bernama lilimnukuu waziri uchukuzi nchini humo Liow Tiong Lai, akisema kuwa mabaki ya ndege hiyo yatafanyiwa uchunguzi kubainia ikiwa yana uhusiano na ndege ya Malaysia iliyopotea ya MH370.
Ndege hiyo ya Boeing 777 nambari MH370 ilitoweka 2014 ikiwa na watu 239 muda mfupi baada ya kupaa kutoka Kuala Lumpur ikielekea Beijing.
Hivi majuzi, mabaki ya ndege sawa na hiyo yalipatikana Madagascar lakini baada ya uchunguzi ikabainishwa kwamba hayakuwa ya ndege hiyo ya MH370.
chanzo: BBC
No comments
+255716829257