Habari mpya

ILE COLLABLE YA MAYUNGA NA AKON ULIYOISUBIRI KWA HAMU MAMBO HADHARANI LEO..

Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star mwaka 2015, Mayunga, anatarajia kuuvunja ukimya wake wa miezi kadhaa kwa kuachia wimbo wake unaosubiriwa kwa hamu, Please Don’t Go Away aliomshirikisha, Akon.
13248793_1598146887163552_2120162996_n
Wimbo huo aliurekodi mwaka jana baada ya kwenda Marekani kukutana Akon aliyekuwa mentor kwenye shindano hilo mwaka jana. Mwaka huu nafasi yake imechukuliwa na Keri Hilson.
Kupitia ushindi huo Mayunga alishinda mkataba wenye thamani ya $500,000 ambazo ni ya zaidi ya shilingi milioni 900 za Tanzania na kuwa chini ya usimamizi wa Universal Records. Nchi 13 zilishiriki kwenye shindano hilo.
Mayunga ambaye Jumapili hii amesherehekea siku yake ya kuzaliwa amesema wimbo huo utachezwa mara ya kwanza kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.
Jikumbushe picha za ushindi wa Mayunga.
chanzo: Bongo5
Mayunga-akiimba-kwa-hisia-kali-kusherehekea-ushindi-wake-
Mayunga-akiwa-amepoteza-fahamu-kwa-muda-
Mayunga-akiwa-haamini-kama-jina-lake-ndio-limetajwa-kama-mshindi-wa-shindano-hilo
RadekArtPhoto-5775
RadekArtPhoto-6102
RadekArtPhoto-6340

No comments

+255716829257